Utamaduni wa Mwamko wa Kijamii

$5.00

Description

Jamii haitavuka hali yake ya kutokuendelea maadamu  watu wake hawajashiba utamaduni  unaowasukuma kuelekea kwenye mabadiliko  na mwamko. Hiyo ni kwa sababu nyuma ya kila hali inayoishi nayo jamii kuna utamaduni  unaoimarisha hali hiyo kwa na kuutetea na kuuhami.

Qur’ani Tukufu imeshaeleza ukweli huu dhahiri shahiri kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyopo kwa watu hadi wabadilishe yaliyomo katika nafsi zao.” (Sura al-Ra’ad: 13:11). Na yaliyomo katika nafsi ni utamaduni ambao unatengeneza hisia na kutengeneza misimamo ya kitabia.

Ujumbe wa mbinguni ulikuwa unawakilisha utamaduni wa mabadiliko na mwamko ambao walikuja nao Manabii kwa umma zao ili kuamsha yaliyofichikana katika akili zao  na ili kukomboa  matakwa yao kutokana na minyororo na hali ya kutoendelea ili waanze kuimarisha ardhi na kujenga jamii tukufu yenye maendeleo.

Haya na mengine utayapata ndani ya kitabu hiki na kuongeza upeo wako wa maarifa katika Uislamu na kijamii kwa ujumla.

Additional information

Weight 0.185 g
Mwandishi:

Sheikh Hasan Musa al Saffar