Utamaduni Kufuatana na Qur’ani na Utekelezaji wa Kivitendo (Sehemu ya 1)

$5.00

Categories: ,

Description

Kama ambavyo Mwenyezi Mungu aliwatuma Manabii na Mitume ili kumkumbusha huyu mwanadamu na kumzindua na kumtoa katika hali za kughafilika na ujinga, “Mitume [ambao ni] wabashiri na waonyaji, [wametumwa] ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, mwenye hekima.” (Sura an-Nisaa’, 4:165)

Mwenyezi Mungu akamtuma Nabii Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.) kama ni Mtume wa mwisho na mbora kuliko manabii wote. Akamteremshia Kitabu cha mwisho kati ya Vitabu Vitakatifu ambacho Qur’ani Tukufu. Kitabu hicho ambacho Mwenyezi Mungu Mwenyewe amekidhamini kuhifadhika kwake kutokana na kuongezwa au kupunguzwa maneno yote yaliyomo humo, kinatoa mwongozo kwa mwanadamu ambao ukifuatwa humpelekea kwenye ufanisi na mafanikio katika maisha yake hapa duniani na huko Akhera.

Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alikuwa akiwaelekeza Waislamu na akiwabainishia umuhimu wa Qur’ani Tukufu na dharura ya kusoma kwake na kutekeleza kivitendo maamrisho yake, kama alivyosema: “Jifunzeni Qur’ani! Hakika ni mazungumzo mazuri na tambueni humo haki inayoamsha nyoyo. Jiponyeni kwa nuru yake, hakika ni ponyo la nyoyo; na isomeni vizuri, hakika ni visa vyenye manufaa sana.”

 

Additional information

Weight 0.075 g
Mwandishi:

Mahdi Ja'afar Sulail