Description
Kitabu hiki kiitwacho, Kauli Sahihi Zaidi katika Kufafanua Hadithi: “Nimemuona Mola Wangu Akiwa na Sura ya Kijana Mzuri,” ni utafiti uliofanywa na mwandishi juu ya hadithi: “Nimemuona Mola wangu akiwa na sura ya kijana mzuri.”
Hii ni hadithi ambayo hupatikana katika vitabu vingi vya hadithi, lakini kwa mtazamo wa haraka utaona hadithi hii ina mapungufu mengi na haikubaliani na vipimo vilivyowekwa vya kupima usahihi wa hadithi husika.
Katika kitabu hiki mwandishi amefanya utafiti wa kina juu ya hadithi hii kwa kutumia ushahidi uliopo kwenye Qur’ani, hadithi na matukio ya kihistoria, na kufikia hitimisho zuri la kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na dhana hii ya kishirikina.
Sisi kama wachapishaji, tunakiwasilisha kitabu hiki kama kilivyo kwa wasomaji wetu na kuwashauri wasome yaliyomo kwa makini, wayafanyie kazi na kuyazingatia, na kufaidika na hazina iliyoko ndani yake.