Description
Mwanadamu anaishi katika ulimwengu huu na anaingiliana na kila anachokutana nacho katika maisha yake. Yapo mahusiano mbalimbali kati ya mja na Muumba wake, kati ya watu wengine na yeye binafsi, kati ya mtu na mtu, ikiwa ni pamoja na familia yake mtu, jumuiya na Umma, na baina ya mwanadamu na viumbe vingine, vyenye uhai na visivyo na uhai vyote. Maamiliano yote haya yanahitajia utaratibu na marekebisho kwa njia ya kuweka maelekezo kwa ajili ya kuongoza mwenendo wa mwanadamu. Hivi ni ili kwamba kila mahusiano ya mwanadamu, yawe ya kibinafsi, kifamilia, kijumuiya au kitaifa, hatimaye yamwongoze kwenye furaha na ustawi.
Sheria zilizotungwa ambazo zimeweka mfumo wa kuelekeza mwenendo wa kitabia wa mwanadamu ndio hukm ambazo ni kisheria za Kiislamu zinazozingira nyanja zote za mwenendo wa binadamu katika ulimwengu huu.