Description
“Ni jambo la wajibu juu ya kila mtu kujifunza mas’ala ambayo yanamtokea mara kwa mara.” Hii ni kauli ya wanavyuoni wa kifikihi iliyodondolewa kutoka vitabu vya fatwa au hukumu za kifikihi.
Hakika kipindi cha ujana kinahesabika kuwa ndiyo fursa yenye thamani katika kujipatia maarifa na kuyavuta kutoka kwenye vyanzo vya elimu ambavyo mtu atafaidika navyo muda wote wa uhai wake.
Kila umri wa mwanadamu unavyosonga mbele, ndivyo majukumu yake yanavyozidi na maisha yake kuwa na msongamano. Kwa hali hiyo, basi hukosa fursa ya faragha itakayomruhusu kujifunza yale yanayomlazimu miongoni mwa hukumu za sharia za Kiislamu, na maoni ya wanavyuoni wa sharia, ambazo nyingi miongoni mwa hizo huenda atazihitajia katika maisha yake hapo baadaye.
Bila shaka mwanadamu anahitaji kuwa na wigo katika kufanya mabadiliko ya kibinadamu ndani ya safari yake ya maisha